... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ratiba ya Mungu Haina Makosa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Habakuki 2:3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Nikisema kweli, mara nyingi sikupendezwa na ratiba yake Mungu.  Mara nyingi zaidi, mateso yaliendelea kupita kiasi.  Halafu, mara nyingi sana amezuia baraka zake muda mrefu pia!  Wewe unaonaje?

Nina rafiki kijana aliyeoa hivi karibuni na baada ya wao kufunga ndoa, mke wake alishikwa na ugonjwa wa kuishiwa nguvu daima.  Kuugua ni kawaida lakini kwa nini Mungu anaruhusu hali hiyo iendelee tu?

Bila shaka wewe na mimi tungeweza kuorodhesha mifano mingi kama huo au mibaya zaidi, ambayo yanasababisha tumtilie Mungu mashaka.  Kwa nini ratiba yake mara nyingi haieleweki kwetu?

Katika Agano la Kale, Nabii Habakuki naye pia alikuwa na malalamiko kama hayo.

Habakuki 1:2  Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia?  Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.

Wakati ule mambo yaliwawia vigumu Waisraeli.  Watu wa Babeli walikuwa wanaleta ghasia.  Isingetushangaza kusikia Habakuki anavyomlilia Mungu.  Jibu lake Mungu lilikuaje?

Habakuki 2:3  Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

Ukizingatia mahali ulipo leo hii, sijui kama ni neno ambalo unalotaka kusikia.  Inategemeana.  Labda hutaki kuamini ahadi ile.  Lakini subiri kwanza.  Mungu anajua kabisa yale ambayo unayapitia.  Na ni faraja kubwa kujua kwamba ratiba yake daima haina makosa.  

Ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.   

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.